Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa wachezaji wake wanatakiwa kupambana kila wanapocheza na timu zilizo nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi kuu nchini uingereza.

“Kama tunahitaji kutwaa ubingwa au kufanya vizuri kwenye ligi lazima tukubali kupambana na Liverpool, Spurs, Manchester City na timu nyingine zote kubwa.

“Wachezaji wangu wanapaswa kupambana sana kila wanapocheza na hizi timu sita za juu,” amesema.

Chelsea ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi zake 26 nyuma ya pointi 11 ya Liverpool waliopo kileleni.

Timu hiyo ilichapwa mabao 2-1 na Manchester City mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Uwanja wa Etihad.

Dante azua mapya Yanga
Jux ''siwezi kumuongelea vibaya Vanessa Mdee''