Rais wa zamani wa FC Barcelona Joan Laporta amejitokeza hadharani na kutangaza dhamira yake ya kuwania tena kiti hicho, kupitia uchaguzi unaoatarajiwa kufanyika klabuni hapo.

Laporta mwenye umri wa miaka 58 aliiongoza FC Barcelona kama Rais, kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010, ambapo katika kipindi chote cha miaka saba ya utawala wake klabu hiyo ya Camp Nou ilipata mafanikio makubwa ndani na nje ya Hispania.

Akiwa Rais wa klabu hiyo Barca ilitwaa mataji mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mataji manne ya Ligi Kuu Hispania (La Liga), chini ya utawala wa meneja kutoka nchini Uholanzi Frank Rijkaard na badae Pep Guardiola raia wa Hispania.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari Hispania imeeleza kuwa: “Kuwa rais wa FC Barcelona ni heshima na ilinipa miaka bora zaidi katika miasha yangu na kurudi tena kuwa rais ni changamoto kubwa katika maisha yangu.” Laporta alisema siku ya Jumatatu.

“Kama wajumbe wataniamini, na shawishika kusema tutarudi katika ubora wetu, tutafanya huku tukiwa na imani na sisi wenyewe.

Ujio wa Rijkaard na Ronaldinho katika mwaka alichaguliwa Laporta uliifanya apate mafanikio makubwa kama kupata ubingwa wa ligi mfululizo mwaka 2004-05 na 2005-06 bila kusahau ubingwa wa Champions League mwaka 2006.

Laporta pia alimleta Pep Guardiola kuwa kocha mkuu wa timu ya wakaubwa ya Barcelona mwaka 2008 maamuzi ambayo yalipelekea klabu kushinda mataji makubwa matatu ndani ya msimu mmoja.

Sababu kubwa ya uchaguzi mkuu klabuni hapo kutarajia kufanyika, imetokana na Rais aliepita Romeo Bartomeu na bodi ya uongozi kujiuzulu mwezi Oktoba siku chake, kabla mashabiki na wanachama wa Barcelona hawajapiga kura kukosa imani viongozi hao.

DFB kumpa ushirikiano Joachim Low
Kiongozi wa Tigray amtaka Abiy kuondoa majeshi