Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, imefuta ratiba za mabasi 38 ya New Force yanayoanza safari zake alfajiri kufuatia mfululizo wa ajali za usafiri huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, CPA. Habibu Suluo amesema kati ya hayo mabasi 10 ni yale yanayoanza safari saa tisa alfajiri na mabasi 28 ya safari za saa kumi na moja alfajiri ambapo ndani ya wiki nne mabasi matano yalipata ajali.

Amesema, “madereva wengi wanaofanya safari za asubuhi hawazingatii alama za barabarani, hivyo tumejadiliana nao na tumefikia maamuzi ya kusitisha safari zao za alfajiri na sasa watalazimika kuanza safari zao kuanzia saa 12 asubuhi.”

Aidha, Suluo ameongeza kuwa LATRA imeshindwa kuwatambua madereva waliokuwa wanaendesha mabasi hayo, ili kuweza kuwachukulia hatua au kupeleka taarifa zao Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, ili wawajibishwe kwa mujibu wa Sheria.

Jose Mourinho kumrudisha dimbani Greenwood
Mo Dewji alivyomng'oa Sawadogo Simba SC