Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini – LATRA, imeongeza muda wa usajili wa Madereva wa miezi mitatu, ikibatilisha agizo la mwisho wa usajili wa Aprili 30, 2023 ambapo sasa zoezi hilo litaendelea hadi Julai 30, 2023.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa LATRA, Jahansen Kahatano ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hadi sasa Madereva 3,334 wamesajiliwa kwenye mfumo idadi ambayo hairidhishi.

Amesema, “tumeona tuongeze muda wa usajili wa Madereva wote nchini kutokana na awali zoezi hili la usajili kuwa na changamoto za Madereva wengi kukosa vyeti vya uereva, wengi wamekosa mafunzo lakini hitaji la kupima Afya, kwa sasa tumeliondoa.”

Hata hivyo, Kahatano amebainisha kuwa ili Dereva aweze kusajiliwa na LATRA anatakiwa kuwa na leseni ya udereva, kadi ya NIDA na cheti cha udereva na wahusika wote wanapaswa kusajiliwa na Mamlaka hiyo kwenye Mfumo wa Kufuatilia Mwenendo wa Magari, VTS.

Mapafu ya Mbwa kupanda ulingoni Juni 30
Yamal Ebana atabiriwa makubwa FC Barcelona