Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay, Edinson Roberto Cavani Gómez huenda akaondoka nchini Ufaransa mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kauli nzito iliyotolewa dhidi yake na meneja wa klabu ya PSG, Laurent Blanc.

Blanc ameonyesha kuwa tayari kumuona Cavani akiondoka kikosini mwake katika majira ya kiangazi, kutokana na mipango yake kutomuhitaji na anaamini huenda ikawa suluhisho la kunusuru kipaji chake cha soka.

Blanc ameonyesha kutokua na maelewano mazuri na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, kwa kukiri wazi uwepo wa tofauti baina yao, hivyo anaamini suluhisho ni kumruhusu kuondoka.

Hata hivyo meneja huyo kutoka nchini Ufaransa, hakuweka wazi ni jambo gani ambalo linaendelea kati yake na Cavani zaidi ya kusisitiza suala la kumpa nafasi ya kuondoka ili kunusuru uwezo wake mkubwa wa kucheza soka.

“Kuna tatizo dhidi ya Cavani, na kwa uzoefu wangu mkubwa katika ufundishaji wa soka ninaamini suluhisho ni kuondoka kwa mchzaji huyu ambaye anahitajika kwenye klabu kadhaa za barani Ulaya,” Alisema Blanc.

Cavani amekua na msimu wa kawaida kutokana na kutochezeshwa mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha PSG, kwani mpaka sasa amepata nafasi ya kujumuika na wenzake mara 24 na kufanikiwa kufunga mabao 13.

Hisia za walio wengi zinamtazama mshambulaiji nguli wa PSG kwa sasa, Zlatan Ibrahimovic kama kikwazo kwa Cavan kucheza mara kwa mara kama ilivyokua inatarajiwa wakati akisajiliwa mwaka 2013 akitokea SSC Napoli ya nchini Italia.

Zilizochukua Nafasi Magazeti Ya England Leo
Gor Mahia Wakamilisha Usajili Wa Nahodha Wa Amavubi