Nahodha na beki wa pembeni wa maafande wa Jeshi la Magereza (Tanzania Prisons) Laurian Mpalile, amefichua siri ya maisha yake, na sababu zinazomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wakongwe wanaoendelea kutumika kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania Bara.
Mpalile ambaye amedumu Tanzania Prisons kwa zaidi ya misimu mitatu, amesema siri ya kuendelea kuwa Fit ni kufanya mazoezi, na kuepukana na starehe ambazo zimekua kikwazo kwa wachezaji wengi hapa nchini.
Siri nyingine iliyowekwa wazi na beki huyo ni kukubali kukosolewa na kupokea ushauri, kutoka kwa wachezaji, makocha na wadau wengine wa soka, ambao anaamini wamekua kama kioo cha kuangalia matatizo yake ya ndani na nje ya uwanja.
Hata hivyo Mpalile akawataka wachezaji wnaaochipukia katika medani ya soka hapa nchini kuhakikisha wanafuata misingo ya kujitunza sambamba na keheshimu mazingira yanayo wazunguuka.
Amesema endapo mchezaji utapenda nachokifanya, kudumisha nidhamu, kuepuka starehe, kutokulewa sifa, kufanya mazoezi na kukubali kukosolewa/Kupokea ushauri, atakua na njia nzuri ya kufurahia maisha yake ya soka kwa muda mrefu.
Penda Unachokifanya
“Kilichonifanya nidumu kwenye mpira kwa muda mrefu kwenye kikosi cha Tanzania Prisons, kwanza kabisa ni kuupenda mchezo wenyewe wa mpira. Naamini ili ufanikiwe katika kazi yako kwanza lazima upende unachokifanya, kwa hiyo mimi niliupenda mpira.”
Nidhamu:
“Kitu kingine kilichonifanya nidumu ni nidhamu ya mchezo wa mpira wa miguu, nidhamu imechukua sehemu kubwa kwa sababu mchezo huu unataratibu zake na miiko yake.”
Epuka Starehe:
“Kama unavyojua starehe kwa mchezaji hazitakiwi, moja ya kitu kinachofanya wachezaji wengi washindwe kudumu ni kwa sababu ya kuendekeza starehe.”
Usilewe Sifa
“Kutokulewa sifa kumenifanya mimi nidumu kwenye mpira. Wachezaji wengi wamekutwa na tatizo la kulewa sifa na kusahau walikotoka matokeo yake wameshindwa kukaa kwenye mpira.”
“Kabla ya kuanza kufanikiwa unakuta wengi wanakuwa na nidhamu ya kufanya mazoezi, kusikiliza walimu na watu wanaokuzunguka lakini mafanikio yanapoanza kuja wengi wanajisahau wanashindwa kuendelea na nidhamu waliyoanzanayo.”
Fanya Mazoezi
“Hakuna uchawi kwenye mpira zaidi ya mazoezi, kadiri unavyofanya mazoezi ndio unavyokuwa fit unapokuwa fit unajiepusha na majeraha yasiyo ya lazima. Hata ikitokea ukapata majera unapona kwa haraka.”
Kubali Kukosolewa/Pokea Ushauri.
“Kukubali kukosolewa, unapokuwa mchezaji lazima ukubali kukosolewa na watu tofauti (waandishi, wachezaji wenzako, walimu) ukikubali kuyapojea na kufanyia kazi ndio kumenifanya nidumu kwa muda mrefu sana.”