Klabu ya Inter Milan ya Italia ipo tayari kumuuza mshambuliaji wake kutoka nchini Argentina Lautaro Martinez, kwa Euro milioni 90 mwishoni mwa msimu huu 2021/22.
Tayari klabu za Liverpool (England), Atletico Madrid (Hispania) na Borussia Dortmund (Ujetrumani) zinatajwa kupigana vikumbo kuiwania saini ya Mshambuliaji huyo.
Martinez alisajiliwa kwa Euro milioni 25, Julai mwaka 2018 kutoka Racing na kuongeza mkataba wake Oktoba 2021 utakaodumu hadi Juni mwaka 2026.
Mshambuliaji huyo amefunga mabao 12 katika mechi 33 za mashindano yote akiwa na Inter Milan msimu huu, lakini ameshindwa kufunga bao katika mechi saba zilizopita za Serie A.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Martinez atauzwa kwa euro milioni 90, ikiwa imepunguzwa kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye kifungu cha mkataba wake cha kumwachia kwa euro milioni 110.
Awali mchezaji huyo alikuwa akihusishwa na mpango wa kutakiwa Barcelona, lakini dili hilo likashindikana.
Na sasa Liverpool inaonekana ipo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsajili ingawa inakabiliwa na ushindani kutoka Atletico Madrid na Borussia Dortmund.