Rais wa Lebanon, Michel Aoun amekataa shinikizo la kujiuzulu kutokana na madai ya uzembe ya mlipuko uliotokea nchini humo ambapo amesema suala hilo haliwezekani kwa sababu litaacha ombwe la uongozi nchini humo.

Rais Auon amesema uchunguzi unaoendelea umegawanywa kwenye hatua tatu na utahitaji muda zaidi kuweza kubaini kikamilifu kilichotokea kabla ya kufikia hitimisho.

Hadi sasa chanzo cha moto uliozuka kwenye ghala lililohifadhi maelfu ya tani za milipuko katika bandari ya Beirut bado hakijulikani ambapo mlipuko huo uliua Watu zaidi ya 180 na kujeruhi maelfu.

Taarifa za Lebanon zinasema viongozi wa juu wa Nchi hiyo akiwemo Rais Aoun walifahamu uwepo wa hifadhi hiyo ya milipuko lakini hawakuchukua hatua.

Mganda kusajiliwa Simba Queens
VPL 2020/21: Simba kuanzia ugenini