Chama cha soka Uingereza (FA) kimemtangaza Lee Carsley kuwa kocha mkuu wa muda wa timu ya taifa.Lee anachukua nafasi iliyoachwa wazi na kocha Southgate aliyetangaza kujiuzuru baada ya kumalizika kwa michuano ya EURO 2024 na kushindwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa miaka miwili mfululizo licha ya kufika hatua ya fainali mara zote.
FA imesema Lee Carsley ataiongoza timu ya taifa kipindi chote cha majira joto wakati wao wanaendelea na uchaguzi wa mrithi sahihi wa Southgate.kocha huyo ataiongoza Uingereza katika michezo dhidi ya jamhuri ya Ireland na Finland katika kinyang’anyoro cha kufuzu michuano ya UEFA NATIONAL LEAGUE.
LEE CARSLEY NI NANI?
Carsley ni mchezaji wa zamani na raia wa taifa la uingereza. lee alivitumikia vilabu vya Derby county, Blackburn rovers, Coventry country, Everton na alistaafu soka mwaka 2011 kama mchezaji wa Coventry City na baadaye alijiunga na benchi la ufundi la timu hiyo kisha kukabidhiwa majukumu kama kocha wa mpito.
Mwaka 2015 alijiunga na Brentford kama kocha mkuu na mwaka 2017 Aliteuliwa tena kuwa kocha wa mpito wa Birmingham city.
Ubora wa kocha huyo ulipelekea kocha huyo kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa vijana wa timu ya taifa ya uingereza (U20) kwa mwaka 2020 hadi 2021.
Mwaka 2021 alipandishwa daraja na kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya (U 21) ya Uingereza.
wakongwe wanasemaje kuhusu lee
Wayne Rooney mchezaji wa zamani wa Uingereza na Manchester United amenukuliwa akisema “nilitamani Pep Guardiola achukue mikoba ya Southgate lakini kama atapatikana kocha wa mpito ndani timu litakuwa Jambo jema”
Wayne Rooney anaamini Guardiola aliyebakiza mwaka mmoja ndani ya Manchester city ni kocha sahihi kwa timu hiyo kuelekea Kombe la dunia la mwaka 2026.
Rooney aliendelea kwa kusema “lee namfahamu vizuri kwa vile tumetumikia pamoja timu ya Everton tukiwa vijana .NI mtu mzuri na kocha mzuri hivyo anastahili nafasi hiyo . Amefanya vyema akiwa na timu za vijana kama ilivyokuwa kwa Gareth Southgate ”
Mategemeo kwa waingereza
Wengi wanaamini kocha huyo ataiongoza timu ya taifa kwa kipindi kifupi na kipimo cha awali ni kuita timu ya taifa tarehe 29 agosti dhidi ya Finland,ugiriki na Ireland. Kocha huyo ataiongoza timu hiyo katika michezo 6 na kama atapata matokeo chanya basi atajihakikishia nafasi ya kusalia kama kocha mkuu.