Ligi kuu ya Uingereza iliendelea tena usiku wa kuamkia leo ambapo Leicester City walikua wenyeji wa Manchester City mchezo uliochezwa katika dimba la King Power na kushuhudia timu hizi mbili zikitosha nguvu kwa kwenda sare ya bila kufungana.

Man City ndio waliotawala mchezo huo kwa asilimia 61, huku wenyeji Leicester wakimiliki kwa asilimia 39.

Wachezaji wa Man City Aleksandar Kolarov ,Kevin De Bruyne, Eliaquim Mangala walipewa kadi za njano huku Marc Albrighton wa Leicester nae akipewa kadi ya njano na mwamuzi Craig Pawson.

Ligi hiyo itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa, Paka Weusi wa Sunderland watawaalika Majogoo wa Jiji la Anfield katika dimba la Light.

Tajiri Kijana Aipasua Simba Kwa Kauli Tata
Wekundu Wa Msimbazi Simba Waigomea Etoile Du Sahel

Comments

comments