Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) amekosoa uteuzi wa Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Jana, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Felix Ntibenda na kumteua Gambo kushika nafasi hiyo akitarajiwa kuapishwa rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia uteuzi huo, Lema amesema kuwa Gambo hakustahili kupewa nafasi hiyo kutokana na namna alivyokuwa akifanya kazi alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.

“Hajui taratibu, amefanya makosa mengi kinyume cha taratibu wakati akiwa Mkuu wa Wilaya, hakustahili kuteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa,” Lema anakaririwa na gazeti la Nipashe.

Aliongeza kuwa alifahamu atapewa nafasi ya kuwa Mkuu wa Mkoa na kwamba anachokifanya yeye ni kuvuruga amani katika eneo hilo.

“Alipokuwa Mkuu wa wilaya ya Arusha, Nilijua anakuja kuvuga amani iliyopo, nilijua kitu kinachoendelea. Nilijua amekuja kuvuruga amani,” alisema Lema.

Lema alikuwa katika mgogoro na Gambo akimtuhumu kuingilia maamuzi ya vikao vya Baraza la Madiwani.

Video: Wanafunzi hewa kusakwa nchi nzima
Jose Mourinho Kumbembeleza Zlatan Ibrahimovic