Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetupilia mbali rufaa ya kupinga maamuzi ya kumnyima dhamana mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema yaliyoamuliwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi.

Maamuzi hayo yamefanyika leo Desemba 2, 2016 ambapo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Anjelo Rumisha amesema kwamba rufaa hiyo ilikuwa imekatwa nje muda uliopangwa.

Baada ya maamuzi hayo, wakili wa Lema, John Malya amesema wameongea na Lema na amewataka wasishughulike tena na kesi hiyo hadi pale upande wa Jamhuri utakapoamua lakini wao wataendelea kukutana na jopo la mawakili ili kuja na njia mbadala

Serikali yapiga marufuku uchapaji holela wa vitabu
Mpango: Wahasibu wabadhirifu watajwe