Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amekamatwa nchini Kenya baada ya kudaiwa kuingia nchini humo kinyume na taratibu.

Lema amekamatwa katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya akiwa ameambatana na familia yake ambapo kwa mujibu wa wakili wake, Lema alikuwa akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda.

Kukamatwa kwa Lema nchini Kenya kunakuja siku chache baada ya mwanasiasa wa upinzani Tundu Lisu kuomba hifadhi katika makazi ya ubalozi wa Ujerumani jijini Dar es Salaam kwa kuhofia usalama wake.

Wakili wa Lema ameongeza kuwa kushikiliwa huko kwa Lema hakuhusiani kwa vyovyote vile na masuala ya kisiasa.

JPM awatoa hofu watendaji wanaohisi kuondolewa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 9, 2020