Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema  amesema kuwa yeye hawezi kupigana na Meya wa Ubungo, Boniface Jacob kwa masuala ya siasa.

Ameyasema hayo mara baada ya kutoka katika kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichokuwa kinatathmini uchaguzi mdogo wa madiwani uliopita.

Amesema kuwa kuna tetesi nyingi kuhusu utabiri alioutoa kuhusu mwanachama mwenzie na mbunge Kibamba, John Mnyika kuhusu kuhama chama hicho.

“Hapo majuzi nilitoa utabiri wangu, na nikasema kuwa kuna baadhi ya wabunge wa Chadema watakihama chama chetu, kwa sasa siwezi sema chochote baada ya kikao hiki cha kamati kuu, tusubiri mwenyekiti ndio atakayetoa mstakabari wa kinachoendelea,”amesema Lema

Hata hivyo, ameongeza kuwa hana ugomvi wowote na mbunge wa jimbo la Kibamba, John Mnyika kama taarifa zilijvyoenea katika miyandao ya kijamii.

Mudathir Yahya mchezaji bora Novemba
Ronaldo atwaa tuzo mchezaji bora wa dunia 2017