Jeshi la Polisi mkoani Arusha limepiga marufuku mikutano ya mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema iliyokuwa ianze leo kwa maelezo kuwa kuna maandalizi ya mtihani wa darasa la saba na mbio za Mwenge wa Uhuru

Taarifa kutoka Ofisi ya Mkuu wa polisi, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) E.Tille wilayani Arusha, amesema katika barua yake iliyothibitishwa na Kamanda wa polisi Arusha, Charles Mkumbo imesema kuwa, Lema amezuiwa kufanya mikutano iliyokuwa imepangwa kuanzia leo hadi Septemba Mosi

“Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha inakutaarifu kuwa imezuia mikutano yako yenye ratiba kuanzia Agosti 27 hadi Septemba 1 kwa ajili ya kupisha maandalizi ya kuhitimisha mtihani wa darasa la saba na Mwenge wa Uhuru,”imenukuliwa barua hiyo

Hata hivyo, Kamanda Polisi Mkoani humo, Mkumbo amesema kuwa sababu ya kuzuia mikutano hiyo ni polisi kuhitajika kwa ulinzi, hivyo haiwezekani kupata wa kulinda mikutano na kushiriki masuala ya mitihani na Mwenge.

Video: Lissu awataka wanasheria kugoma
Sheikh Salum ataka waliokwamisha mahujaji uwanja wa ndege wakamatwe