Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kutumia busara kuwaondoa bungeni wabunge nane walioingia bungeni kuziba nafasi za wabunge nane waliokuwa wamevuliwa uanachama wa chama cha CUF Julai 24.

Lema ametumia mtandao wake wa kijamii kuandika ujumbe huo ikiwa ni siku moja baada ya Mahakama Kuu kutengua uamuzi wa kufukuzwa kwa Wabunge 8 na Madiwani 2 wa Chama cha Wananch CUF mpaka pale shauri la msingi litakaposikilizwa.

“Mh Spika anapaswa, kuzingatia kwa busara uamuzi uliotolewa na mahakama kwa kuwaondoa wale Wabunge wa Lipumba ndani ya Bunge na kuwarejesha Wabunge halali sasa, Mpaka hapo haki itakaposhinda zaidi,”ameandika Lema

Hata hivyo,Wabunge hao nane walivuliwa uanachama Julai 24 na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama cha Wananchi, CUF linaloongozwa na Prof. Lipumba  kwa madai ya utovu wa nidhamu yakiwemo kukisaliti chama hicho.

Wilder amtia moyo Anthony Joshua kuhusu ‘kumpasua’
Njia bora za kujikinga Kisukari zatajwa