Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, amepata nafasi ya hifadhi ya kisiasa nchini Canada.

Kwa mujibu wa wakili wake George Wajackoyah, Lema aliondoka jana nchini Kenya akiwa na familia yake.

Mwezi uliopita, Siku chache baada ya Uchaguzi mkuu wa Tanzania, Lema aliyeshindwa katika kinyang’anyiro cha Ubunge wa jimbo la Arusha mjini alikamatwa na polisi nchini Kenya kwa tuhuma ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kumuachia huru baada ya muda mfupi.

Baada ya kukamatwa wakili wake, George Wajackoyah, alidai kwamba Lema ambaye alikuwa ameambatana na familia yake alikuwa akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.

Jordi Farre: Messi atasaini mkataba mpya Barcelona
Paolo Rossi amfuata Diego Maradona