Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu sasa inaendelea vizuri ukilinganisha na hali ilivyokuwa hapo awali ingawa bado yupo ICU.

Ameyasema hayo alipokuwa akifanyiwa mahojiano na BBC ambapo amedai kuwa hali ya kiongozi huyo inazidi kuimarika ukilinganisha na siku za awali ambazo alikuwa amefanyiwa shambulio hilo.

“Mgonjwa anapokuwa yupo hospitali tena kwenye chumba cha wagonjwa mahututi huwezi kusema hali ya mgonjwa ni nzuri, lakini kwa kadri ambavyo tumekuwa hapa Nairobi kwa siku zote mimi na wenzangu akiwepo Mchungaji Msigwa, mke wa Lissu na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe tunaweza kusema kuna mabadiliko lakini bado Tundu Lissu yupo ICU na ni wito wetu kwamba Watanzania wote wenye mapenzi mema waendelee kumuombea,” amesema Lema

Aidha, amesema kuwa jaribio la kutaka kumuuwa Lissu ni mpango na watu waliofanya hivyo wala siyo majambazi bali walifanya hivyo kwa lengo la kutaka kutuma ujumbe kuwa wanaweza kufanya lolote na wasifanywe chochote.

Hata hivyo, Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Mjini Dodoma na baadaye kupelekwa nchini Kenya kwaajili ya kupatiwa matibabu

Kevin De Bruyne amjaza kiburi Pep Guardiola
CUF inahitaji maombi- Kumbilamoto