Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa suala la haki, usawa na utawala wa sheria haliwahusu Chadema peke yao bali ni wajibu wa kila mwananchi.

Ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii ambapo amedai kuwa tatizo kubwa linalolikabili taifa kwasasa ni kuwa wananchi wanadhani kuwa haki na demokrasia inatafutwa na wapinzani pekee.

“Watu wanafikiri masuala ya haki, usawa na utawala wa sheria ni wajibu wa CHADEMA hawa wana hitaji maombi na dua, jambo lolote linalohusu haki na demokrasia ni wajibu wa kila Mwananchi. tatizo kubwa linalokabili nchi kwasasa ni kuwa na aina hii ya fikra hata kwa wanaoitwa wasomi,” ameandika Lema.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Lema imekuja ikiwa ni siku moja toka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA), Freeman Mbowe kudai kuwa hawaridhishwi na mwenendo wa kesi inayowakabili

 

Video: Mimi napambana kwaajili ya Rais Dkt. Magufuli tu- Musiba
Congo DRC yawakataa wasimamizi wa uchaguzi wa Kimataifa