Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amesema kuwa viongozi wa Chama hicho wanavumilia mateso mengi wanayopitia katika vita ya Demokrasia.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha Kamati Kuu kilichoitishwa kwa dharula ili kuweza kutoa msimamo wa chama chao, kutokana na viongozi wao wa nafasi za juu akiwemo, Freeman Mbowe kulala Segerea na kunyimwa dhamana katika kesi zao zilizosomwa jana.

“Muelewe tu kwamba hii vita sio ya CHADEMA bali hii vita ni ya Demokrasia, hata sisi tukisema tunaiacha siasa vita hii itaendelea tu. haya mashaka tunayavumilia kwasababu ya msingi ya vizazi na nchi yetu, ndio sababu kubwa tunavumilia mateso na udhalilishaji. lakini nafikiri sasa inatosha,”amesema Lema

Hata hivyo, amedai kuwa hayo mambo yanayoendelea kutokea hasa katika chama chao anayajua vizuri huku akisisitiza kuwa kuna asilimia kubwa kesho viongozi wao wa nafasi za juu wa Chadema kukosa dhamana.

 

Serikali, Mahakama zazidi kuvutana kuhusu Miguna
Shein awaapisha viongozi leo