Aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ambaye mwaka jana alihama CCM na kujiunga na Chadema kabla ya uchaguzi mkuu, jana alihudhuria mkutano wa hadhara wa Rais John Magufuli uliofanyika mjini hapo na kuzungumza naye.

Lembeli ambaye alionekana kuwa mbunge machachari akiwa CCM na aliyejipatia nguvu zaidi kwa wananchi baada ya kuongoza Kamati iliyochunguza ‘Opereseheni Tokomeza Ujangili’, alimweleza mkuu wa nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Dkt. John Magufuli kuwa yuko tayarudia chama hicho endapo atakisafisha.

“Niko hapa kama Lembeli, na watu wasiitafsiri vinginevyo. Nipo hapa kwa sababu kazi unayoifanya sasa mheshimiwa Rais ndiyo kazi niliyokuwa naipigania miaka kumi nilipokuwa mbunge wa jimbo hili,” alisema.

“Niseme kuwa nilitoka kwenye chama chako kwa sababu  ya unafiki, rushwa, ufisadi, ulikuwa umetamalaki katika mkoa huu wa Shinyanga,” aliongeza na kusisitiza kuwa endapo Rais Magufuli atakisafisha chama hicho yuko tayari kurejea na kwamba hata akimtuma kufanya kazi hivi sasa yuko tayari.

Rais Magufuli kumshauri mwanasiasa huyo kurejea ndani ya chama hicho huku akimuahidi kutomkata mkia kama alivyowahi kusema kwani anajua uwezo wake kiutendaji huku akibainisha urafiki wao.

“Wana Kahama tambueni kuwa Lembeli ni rafiki yangu wa siku nyingi na kuwepo kwake hapa ninategemea mabadiliko makubwa kutoka kwake. Na nakushauri [Lembeli] urudi CCM kwani kwa sababu ulikokwenda ulikuwa umepotea,” alisema Rais Magufuli.

Rais Magufuli aliusifia utendaji kazi wa Lembeli na kumuahidi kuwa endapo atarejea ndani ya CCM hatamkata mkia (hatampunguza nguvu) ya kisiasa ndani ya chama.

Arsene Wenger Aponda Usajili Wa Paul Pobga
Mohamed Dewji Kukutana Na Kamati Ya Utendaji Ya Simba