Kabla ya majina Julia na Martha Stewart kuwa maarufu, kulikuwa na jina la Lena Richard (Septemba 9, 1892 au 1893 – Novemba 27, 1950), huyu alikuwa Mwanamke wa kwanza Mweusi nchini Marekani kuandaa kipindi chake cha mapishi cha Luninga akitokea kutoka jimbo la New Orleans, Louisiana.

Ikumbukwe katika miaka ya 1940, Watu weusi bado walikuwa wakikabiliwa na ubaguzi uliokithiri, lakini hiyo haikuzuia kile ambacho MUNGU amemuandikia mtu kupata mafanikio na kipindi chake kilirushwa hewani kuanzia Oktoba 1949 – Novemba 1950, kwenye kituo cha Luninga cha WDSU.

Lena Richard sio tu kwamba alikuwa na kipindi Luninga, lakini pia alikuwa na Migahawa miwili, biashara ya Vyakula vilivyogandishwa, aliandika kitabu cha upishi kilichouzwa nchi nzima na alifungua shule yake ya upishi, ili kufundisha upishi na uchumi wa nyumbani kwa wapishi weusi.

Kiuhalisia umaarufu wake haukuja kutokana na weusi alionao, bali ulitokana na kwanza kuwa Mpishi, Mwandishi wa Vitabu vya upishi, Mgahawa, Mjasiriamali wa Vyakula vilivyogandishwa na Mtangazaji wa Luninga.

Hapo awali Lena alipata elimu yake ya upishi huko New Orleans na baadaye huko Boston ambapo alihudhuria shule iliyoanzishwa na Fannie Farmer na kuhitimu mwaka wa 1918 na kurudi New Orleans ambapo miaka michache baadaye alifungua biashara yake ya upishi na mikahawa kadhaa.

Lakini pia alifungua shule hiyo ya upishi mwaka 1937 huko New Orleans maalum kwa Wanafunzi Weusi na mwaka 1939, Lena alichapisha kitabu cha Richard’s Cook Book ambacho kilimfanya kuwa Mwandishi wa kwanza Mweusi kuangazia vyakula vya New Orleans Creole.

Nadhani filamu ya hali halisi au wasifu wake inahitaji kutayarishwa juu yake kama ilivyokuwa kwa Julia, ili kizazi hiki kiweze kujifunza namna ambavyo vinapaswa kufanya pale wanapokabiliwa na nyakati ngumu katika utafutaji ili kupata mafanikio.

Bungeni: Mradi kuimarisha Umeme Vitongojini mbioni
Wabunge wapinga pendekezo la Rais, Miradi yatatizika