Mcheza mpira wa miguu, Mhubiri wa amani na upendo, Mwanamapinduzi, Mwanaharakati, Mpiganaji, Mwanasiasa, Mwanamuziki wa Reggae na Nyota ya kwanza katika ulimwengu wa tatu Robert Nesta maarufu kama “Bob” Marley alizaliwa February 6 mwaka 1945 na mama mweusi aliyeitwa Cedella Booker na baba wa Kizungu aliyeitwa Norvall Marley. Wakati akiwa mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani kama ‘Tuff Gong’ na kufariki dunia siku kama ya leo Mei, 11, 1981.
Alianza muziki miaka ya 1960 akiwa na kundi lake la Wailing Wailers, ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza zilizoitwa “Judge Not” na “One Cup of Coffee”.
Bob alimuoa Bi. Rita Anderson mwaka 1966 na akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu.
-
Nchi hii inatia aibu kuagiza mafuta nje ya nchi- Zitto Kabwe
-
Alikiba aipa tano ‘Hapa Kazi tu’ ya JPM
Mwaka wa 1974, pamoja na kundi la Wailers kutengana, Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya huku wakindelea kupiga muziki kama kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimpa umaarufu duniani kote, ulijulikana kama “No Woman No Cry”.
Baadhi ya nyimbo zake kali ni pamoja na “I Shot the Sheriff”, “Could You Be Loved”, “Stir It Up”, “Jamming”, “Redemption Song”, “One Love” na, “Three Little Birds”.
Bob Marley alifariki katika hospitali ya Cedars of Lebanon Hospital huko mjini Miami, Florida, kwa tatizo la melanoma (kansa ya ngozi) iliyoanza kushambulia kidole chake cha mguuni.
Bob Marley aliacha watoto 12, wengi wao wanajihusisha na muziki wa reggae na hip hop.
Bob Marley atakumbukwa zaidi duniani kama balozi na shujaa halisi wa muziki wa reggae. Atakumbukwa kwa kuuweka muziki huu wenye nguvu katika ramani ya ulimwengu.