Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Philip Mpango amepokea gawio la zaidi ya shilingi bilioni 15 kutoka benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya faida iliyopata kwa mwaka 2019.
Miongoni mwa mambo ambayo ameyazungumza ni pamoja na kushukuru taasisi za fedha ambapo amesema magawaio hayo husaidia kuongeza mapato ya serikali.
Waziri Mpango ameeleza kuwa faida hiyo itaelekezwa katika miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi ambapo ameziasa taasisi za fedha kuhakikisha kwamba wanaweka riba ndogo katika mikopo ili kuweza kusaidia wananchi hasa wale wa kipato cha chini.
”Uchumi wetu unaendelea kukua vizuri na mimi ninaimani kabisa kwamba tumeingia kwenye kundi la nchi zenye kipato cha kati hiki ni kiashilia kwamba sekta ya benki inaendelea vizuri..ni wiki iliyopita tu nimepokea gawaio kutoka bank ya CRDB walipata faida, kwahiyo maana yake ni kwamba uchumi wetu unaendelea vizuri na sekta ya fedha ndio kipimo cha jinsi uchumi unavyoenda” amesema Waziri Mpango.