Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Kilele cha Mbio za Mwenge wa uhuru kinamalizika hii leo Oktoba 14, mjini Babati Mkoani Manyara, ambapo Mgeni rasmi Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan anaongoza tukio hilo.

Kilele hicho, kinaambata na ibada ya Misa maalum ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika Kanisa la Katoliki Parokia ya Roho Mtakatifu Babati.

Kauli mbiu ya ilele hicho cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 ni “TUNZA MAZINGIRA OKOA VYANZO VYA MAJI KWA USTAWI WA VIUMBE HAI NA UCHUMI WA TAIFA.

Coastal Union: Tuna imani na Mwinyi Zahera
Fei Toto: Waambieni kitaeleweka Oktoba 25