Mshambuliaji wa klabu bingwa Barani Ulaya FC Bayern Munich Robert Lewandowski ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA, kwa mara ya kwanza kwenye historia ya masiaha yake ya soka.

Lewandowski raia wa Poland alitangazwa kushinda tuzo hiyo, wakati wa hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Alhamis mjini Zurich, Uswizhuku akiwashinda mshambuliaji wa mabingwa wa Italia FC Juventus, Cristiano Ronaldo na nahodha wa FC Barcelona Lionel Messi.

Lewandowski, alikuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kushinda tuzo hiyo kufuatia klabu yake ya FC Bayern Munich kushinda mataji yote matano msimu uliopita, likiwepo taji la klbu bingwa Barani Ulaya.

Mbali na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa FIFA kutangazwa usiku wa kuamkia leo, pia washindi wengine walifahamika ambapo tuzo ya Kipa bora ni Manuel Neuer (Bayern Munich na Ujerumani), Kocha bora ni Jurgen Klopp (Liverpool), tuzo ya FIFA Puskas (Goli Bora) imekwenda kwa  Heung-min Son (Tottenham v Burnley) na tuzo ya Foundation ya FIFA: Marcus Rashford kwa kampeni ya umaskini wa chakula cha watoto.

Kikosi cha bora cha FIFA kwa mwaka 2020 (Wanaume): Alisson; Alexander-Arnold, Sergio Ramos, Van Dijk, Davies; De Bruyne, Thiago Alcantara, Kimmich; Messi, Lewandowski, Ronaldo.

Upande wa mchezaji Bora wa Mwaka kwa Wanawake ni Lucy Bronze (Manchester City na England), Kipa kwa wanawake ni Sarah Bouhaddi (Lyon na Ufaransa), Kocha wa wanawake ni Sarina Wiegman (Uholanzi).

Kikosi bora cha FIFA kwa mwaka 2020 (Wanawake): Endler; Shaba, Renard, Mkali; Rapinoe, Heath, Boquete, Bonansea, Ngumu; Miedema, Cascarino.

Kocha Kaze aitumia salamu Dodoma Jiji FC
Ligi Kuu: Msako wa alama tatu kuendelea