Washambuliaji Robert Lewandowski na Karim Benzema wanaendelea kuchukuana vikali katika vit ya kuwania Kiatu cha Dhahabu katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’.
Lewandowski ambaye anayeitumikia FC Barcelona hadi sasa amefanikiwa kupachika mabao 19 huku Benzema akifunga mabao 17 katika ligi hiyo.
Hadi sasa Lewandowski ameshuka dimbani mara 29 kuichezea FC Barcelona ambayo tayari imshacheza michezo 33, huku Benzema ameshuka dimbani mara 21 katika mechi 33 ya Real Madrid.
Nafasi ya tatu katika orodha ya ufungaji kwenye Ligi ya Hispania ipo kwa Enes Ünal wa Getafe na Joselu wa Espanyol ambao tayari wamepachika mabao 14 kila mmoja.
Nafasi ya nne, Antoine Griezmann wa Atlético Madrid na Álvaro Morata wa Atlético Madrid ambao wanachuana, kwani kila mmoja amepachika mabao 13.
Huku kazi kubwa ikiwa kwa Borja Iglesias wa Real Betis, Vedat Muriqi wa Mallorca, lago Aspaslago wa Celta Vigo na Valentín Castellanos wa Girona wote kila mmoja amefunga mabao 12 hadi sasa.