Kituo cha sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeiomba serikali kuingilia kati kesi ya mtoto Nyanzobhe Mwandu (4) aliyefariki dunia baada ya agizo la nyumba 30 kuchomwa moto katika operasheni ya kuwaondoa waliovamia hifadhi ya jamii Isawima Wilaya ya Kaliua kata ya Usinge Mkoani Tabora.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo Juni 21, 2021 Mkurugenzi wa LHRC Ana Henga ambae pia ni wakili amesema kuwa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Abel Busalama amekiuka masharti ya katiba ya Ibara ya 24 (1) inayosema kila mtu anahaki ya kumiliki mali na kuhifadhi mali yake na kuagiza kuangamizwa kwa nyumba hizo pamoja na mazao na kuiomba serikali kuchukua hatua juu ya Mkuu huyo wa Wilaya.

Aidha ameiomba Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Waziri wa Maliasili na Utalii kufanya ziara kwenye kata hiyo na kusikiliza kero za wananchi juu ya vitendo vya ukatili vilivyofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ili kupataa suluhu ya swala hilo.

Pia wameiomba TAMISEMI kuhakikisha mipaka ya vijiji vilivyopakana na ardhi ya hifadhi inawekwa bayana ili wananchi wafahamu mipaka ya vijiji vyao ilipoishia, hii itasaidia kutatua matukio kama ya marehemu Nyanzobhe.

Mfanyakazi wa ndani amuua mtoto wa bosi wake
Kasimamie ukusanyaji wa mapato - Waziri Ummy