Pande mbili hasimu zinazohusika na mgogogro nchini Libya zimekubaliana kutia saini mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano baada ya kufanyika mazungumzo ya siku tano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa.

Mjumbe mwandamizi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mgogoro wa Libya, Stephanie Williams amesema makundi yenye silaha na vikosi vya kijeshi vimekubali kurejea kwenye kambi zao na kwamba makubaliano yaliyofikiwa yataanza kutekelezwa mara moja.

Shirika la Mafuta la Kitaifa la Libya (NOC) limetangaza kuanza tena kwa usafirishaji wa mafuta kutoka kwenye vituo viwili muhimu mashariki mwa nchi hiyo baada ya pande zinazopingana kuzatangaza kuwa zimefikia makubaliano ya kusitisha mapigano.

Aidha Shirika la Mafuta la Kitaifa limesema kuwa limepokea uthibitisho kwamba vikosi vya kigeni vimeondoka kutoka kwenye eneo la bandari hatua itakayoliwezesha shirika hilo kufanya shughuli zake za kuchimba mafuta na kuanza kuuza nje.

Vituo hiyvo viwili muhimu vya kuzalisha mafuta ghafi ni Ras Lanuf na Al-Sidra, ambavyo vilikuwa vinadhibitiwa na Jenerali Khalifa Haftar.

51 wauawa katika maandamano Nigeria
Ujumbe wa JPM kwa marais wajao