Chama cha soka nchini Libya (LFF) kina imani na ujuo wa viongozi wa FIFA nchini humo na wamesema ujio wao utasaidia taifa hilo kuondolewa kifungo cha kutokuandaa michezo ya soka ya kimataifa katika ardhi yao.
Libya ilifungiwa kuandaa michezo ya kimataifa kufuatia vita ya mwenyewe kwa mwenyewe ya mwaka 2011 na kupelekea timu yao ya taifa kulazimika kucheza michezo yake nje ya nchi hiyo.
Ujumbe wa FIFA ukiongozwa na Mkurugenzi wa maendeleo ya soka kwa vyama vya soka barani Afrika, Veron Mosengo-Omba, ambao utakuwepo katika jiji la Tripoli kwa muda wa siku mbili kuzungumzia maendeleo ya mpira wa miguu nchini humu tangu kufungiwa na shirikisho hilo.
“Uwepo wangu ni mwanzo wa hatua za kurudisha michezo ya kimataifa ndani ya Libya ” amesema Veron Mosengo-Omba.
“sio mimi nitakae toa maamuzi,nitatoa taarifa,kwasababu mimi ni mwakilishi wa raisi wa FIFA,nitawakilisha repoti ya ujio wangu kwake,na kisha FIFA wataamua ni kivipi na lini watarudisha michezo ya kimataifa ndani Libya” ameongeza Veron Mosengo-Omba.
Timu ya Taifa ya Libya kwa miaka mitano iliyopita imekuwa ikicheza michezo yake ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia na mataifa ya Afrika katika nchini Mali, Misri na Tunisia.