Waziri Mkuu wa Libya, Fayez al-Serraj amesema kufungwa kwa miundombinu ya mafuta kunaweza kusababisha mgogoro mkubwa wa kifedha nchini humo.
Amesema kuwa kuendelea kufungwa kwa vituo hivyo kumeleta athari kubwa kwa bajeti ya Serikali ambapo amesema usafirishaji wa mafuta ni chanzo kikuu cha mapato katika nchi hiyo
Al-Serraj ambaye anaongoza Serikali inayoungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa amesema hadi sasa hasara ya zaidi ya Dola Bilioni 1.4 imeshapatikana.
Januari mwaka huu, Waaandamaji wa Mbabe wa Kivita, Khalifa Haftar walifunga mabomba na bandari za kusafirisha mafuta, hali ambayo imesababisha kupungua kwa uzalishaji na usafirishaji wa nishati hiyo.