Lydia mollel – Morogoro.

Wadau mbalimbali wameendelea kuunga mkono jitihada zinazofanyawa na Serikali kwa kutoa  misaada Mkoani Manyara ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na Kampuni ya Viridium Tanzania Limited wameungana kutoa msaada wa majiko 50 pamoja na nishati mbadala wa mkaa mweupe kwa waathirika wa mafuriko.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kwa msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima amesema msaada huo uliotolewa na kampuni ya Viridium kwa niaba ya watu wa Morogoro una thamani ya zaidi ya  shilingi million 10.

Malima amesema, Morogoro inategemea kupeleka msaada Hannag kwa awamu mbili licha ya kuwa Mkoa huo umekumbwa pia na maafuriko Wilayani Kilosa, yaliyosababisha kaya zaidi ya 150 kupoteza makazi na kifo.

Hata hivyo, maafuriko mengine yametokea katika maeneo mbalimbali ikiwemo Dumila na Kitete usiku wa kuamkia Desemba 8, 2023 na tayari msaada wa chakula umepelekwa na bado wanatetarajia kupeleka misaada mingine, huku Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilosa ikifanya tathmini ya hasara iliyopatikana.

Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Viridium Tanzania Limited, Aristotle Nikitas amesema wametoa msaada huo kwa lengo la kuwasaidia waathirika hao kupata vifaa muhimu kwa ajili ya kupikia.
 
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi – CCM Mkoani Morogoro, Solomoni Kasaba ametoa pole kwa waathirika wa maarufiko Mkoani Manyara na kusema wameungana na Watanzania wengine kwa kutoa msaada wa majiko na mkaa, ili kuwasaidia mahitaji muhimu.

Wananchi washangaa kuona Rais akiomba kura
Vifo vyafikia 80, mipaka yawekwa Jorodom