Ligi kuu ya soka Tanzania bara (VPL) leo ijumaa inaendelea kucheza michezo miwili itakayochezwa katika uwanja wa Namfua mkoani Singida.
Kikosi cha Singida United kitashuka dimbani kuikaribisha Mtibwa Sugar Fc kutoka Manungu mkoani Morogoro.
Singida United inaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kufanikiwa kuitoa klabu ya Yanga kwa mikwaju ya penati kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho.
wakati huo huo, Mtibwa Suger wao pia watacheza mchezo huo huku wakikabiriwa na mchezo mgumu mbeleni dhidi ya Simba utakaochezwa mjini Morogoro Jumatatu ya wiki ijayo.
Aidha,Timu zote zimejinasibu kushinda mchezo huo utakao pigwa majira ya saa 10 jioni, Singida United inakamata nafasi ya 5 katika ligi hiyo ikiwa na pointi 36 ikifuatiwa na Mtibwa Suger yenye pointi 27 .
Mbali na mchezo huo , Mbao FC nayo itakuwa inawaalika Lipuli FC kutoka Iringa katika mchezo utkao chezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.