Patashika ya ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi itaendelea tena hii leo Jumanne na kesho Jumatano, katika viwanja mbalimbali barani humo.
Mabingwa watetezi, Real Madrid watakua wagenini wa APOEL ya nchini Cyprus huku wakimkosa nahodha wao Sergio Ramos ambaye ni majeruhi.
Wapinzani hao wa Madrid hawajashinda mchezo hata mmoja katika Kundi H, hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa mwepesi kwa Madrid ambao wanahitaji ushindi baada ya kutokuwa na matokeo mazuri katika mechi za hivi karibuni.
Michezo mingine ya leo Jumanne.
BeşiktaşvPorto
Spartak MoskvavMaribor
Borussia Dortmund v Tottenham Hotspur
Napoli v Shakhtar Donetsk
SevillavLiverpool
APOEL v Real Madrid
Manchester CityvFeyenoord
MonacovRB Leipzig
Michezo ya kesho Jumatano.
CSKA MoskvavBenfica
QarabağvChelsea
JuventusvBarcelona
BaselvManchester United
Anderlecht v Bayern München
Sporting CP v Olympiakos Piraeus
Atlético Madrid v Roma
PSGvCeltic