Mtangazaji wa 100.5 Times Fm, Omary Tambwe maarufu kama Lil Ommy ametoa jarida maalum la kipindi hicho ‘The Playlist Magazine’, toleo la Mwezi Juni hadi Julai linalopatikana bure kwa ajili ya wasikilizaji wa kipindi hicho.

Toleo hilo limebeba ‘exclusive interviews’ alizofanya na mastaa mbalimbali katika kiwanda cha muziki nchini Tanzania wakiwemo Christian Bella, Meninnah La Diva, Cassim Mganga na Peter Msechu.

Jarida hilo pia limebeba mahojiano ya kibabe yaliyogusa unyeti wa mambo mbalimbali ya warimbwende Maggie Vampire na Tunda.

“Unajua siku zote huwa nawaza jinsi ya kuwapa fans na wasikilizaji wa The Playlist ya 100.5 Times Fm zaidi ya kile wanachokitarajia na hii ndio siri ya kufanya magazine hii kali zaidi ya zilizopita na ofcourse walioiona wanasema ni kali kuliko nyingi zilizopo sokoni,” Lil Ommy ameiambia Dar24.

“Nashukuru sana uongozi wa Times Fm na wafanyakazi wenzangu kuhakikisha tunapata kopi nyingi za kuwapa mashabiki tena bure kabisa. Zinapatikana kwenye maeneo mengi zikiwemo supermarket, Saloon na Maduka makubwa hapa Dar es Salaam. Kwa sasa mikoani linapatikana Tabora, Mwanza, Dodoma, Tanga, Morogoro na Mbeya,” alisema Lil Ommy.

‘The Playlist Magazine’ hutolewa baada ya miezi miwili likibeba mambo makubwa kwenye tasnia ya sanaa nchini na hata duniani kwa ujumla. Toleo hili la mwezi wa Juni – Julai limebeba matukio makubwa ya tuzo za BET na MTV/MAMAs pamoja na story kubwa za mastaa wa Marekani kama Rihanna na Chrisbrown.

“Natamani kila mmoja alipate jarida hili bure kabisa, lakini nakala ziko chache kuliko wasikilizaji au wale ‘die hard fans’ wa Times Fm, so nashauri kila mmoja ajitahidi kuwahi asikose interviews za kibabe ambazo hajazisikia sehemu yoyote,” alisema Lil Ommy.

Kipindi cha The Playlist kinaruka hewani kila Jumapili saa 10 kamili jioni hadi saa 12 kamili jioni kupitia 100.5 Times Fm.

 

 

Peter Msigwa, Lissu Wazungumzia Uamuzi Wa Dk. Slaa
Los Angeles Kuwania Nafasi 2024