Rapa Lil Wayne ameendelea kukumbwa na tatizo la ugonjwa wa kifafa ambapo ameripotiwa kuwa katika hali mahututi wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa TMZ, Lil Wayne alisombwa na kifafa akiwa Las Vegas  alipoenda kufanya tamasha kwenye klabu moja ya usiku Julai 6. Kutokana hali yake kuwa mbaya, aliahirisha tamasha hilo na kukimbizwa hosptalini ambako alilazwa katika chumba cha watu mahututi (ICU).

Hata hivyo, chanzo kimeeleza kuwa aliruhusiwa kuondoka hospitalini hapo siku iliyofuata baada ya kupata matibabu na afya yake kuimarika.

Boss huyo wa Young Money amekuwa akikabiliwa na tatizo hilo tangu mwaka 2012 lilipowekwa rasmi wazi. Ndege yake imekuwa ikitua kwa dharura mara kadhaa baada ya hali yake kubadilika akiwa hewani.

Brazil Yapata Pigo Kuelelea Michuano Ya Olimpiki
Kikosi Bora Cha Euro 2016 Chatajwa