Unywaji wa maji ya uvuguvungu yaliyochanganywa na limao au ndimu humpatia mtu nguvu na kumkinga na magonjwa hatarishi, kutokana na matunda hayo kuwa na utajiri wa vitamin C, pia ndimu ina vitamini B- Cmplex, madini ya Kalsiamu, Chuma, magnesium, potasium na fiba.

Faida ya kunywa maji yenye ndimu au limao:

Kupunguza hatari ya Kiharusi; kutokana na matokeo ya kitafiti ulaji wa matunda jamii ya limao husaidia kupunguza hatari ya kupatwa na shambulio la kiharusi aina ya Ischemic hasa kwa wanawake.

Kurekebisha sukari katika mwili; limao husaidia kuweka kiasi cha sukari tumboni na katika mwili kuwa katika kiasi stahili, hii huwasaidia sana wagongwa wa sukari katika ulaji wao.

Kinga dhidi ya Saratani; vitamini C Antioxidant ambayo inasidia kuondoa mionzi hatari mwilini ambayo imetambulika kusababaisha saratani.

Urekebishaji wa ngozi kupona makovu; limao linasidia kufanya ngozi isizeeke kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia.

Tabia za Vitamini C za kusafisha uchafu zinasababisha kufaya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.

Huyu ndiye Mwanamke Mtanzania wa kwanza kufika kilele cha Mlima Everest
Waliohitimu kidato cha sita waitwa JKT