Madiwani Sita wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi wamejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoka vyama vya upinzani wakidai kuunga mkono Utekelezaji wa Ilani ya CCM bila ubaguzi na kusimamiwa na mkuu wa wilaya hiyo Hashimu Komba aliyeanza kazi miezi michache iliyopita na kuonyesha uwezo mkubwa wa kuwajali wananchi.

Madiwani hao waliojiunga na CCM wakitokea chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) wamebainisha kuwa wamechukua uamuzi huo bila kushawishiwa na Mtu yeyote, baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya CCM ambayo imekuwa ikitatua kero za wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo bila kujali maeneo yanayoongozwa na upinzani.

Madiwani hao kutoka Kata za Naipanga na Mpiruka kupitia CHADEMA na kutoka kata za Kiegei na Namapwia kupitia CUF pamoja na wawili wa Viti maalum kupitia Chadema na Cuf, ni Omari Lingumbende, Hemedi Madongo, Catherine Kapanda, Jamali Mustafa, Esha Mdamo na Gabrieli Matuta. 

Uhuru Kenyatta atangaza mpango wa kuchochea uchumi
Trump aagiza Magavana kufungua sehemu za Ibada