Imefahamika kuwa baada ya FC Barcelona kutwaa taji la Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ msimu huu 2022/23 ambalo walilikosa kwa misimu minne, nguvu kubwa sasa ni kumrejesha Nahodha na Mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi.

FC Barcelona wanatajwa kuwa mbioni kumrudisha, Messi kikosini hapo licha kuwa na umri wa miaka 35.

Kurejea kwa Messi kunatajwa kuwa kunaweza kuwa na faida kubwa kwa FC Barcelona hususan kwenye kuuza jezi na kuongeza viingilio kwenye mechi zao.

Hata hivyo mshindi huyo wa Kombe la Dunia 2022 anatajwa kutakiwa na klabu kutoka Saudi Arabia ambayo imemtangazia kufuru ya mshahara.

Messi amepewa ofa ya zaidi ya Pauni milioni 500 ili kuungana na Cristiano Ronaldo kwenye ligi ya Saudi Arabia, wakati FC Barcelona wameambiwa lazima wapunguze dau lao la mshahara kwa pauni milioni 180.

Messi atakuwa mchezaji huru msimu wa joto kwani atakuwa anamalizana na PSG na Barcelona wanahusishwa kwa ukaribu zaidi tangu alipoondoka kwa miaka miwili iliyopita huku suala la ukata likitajwa kuchangia kuondoka kwake.

Cristiano Ronaldo kurudi Real Madrid?
Meridianbet: Sloti mini Power Roulette ushindi ni rahisi