Hatimaye Nahodha na Mshambuliaji wa Kikosi cha Mabingwa wa Dunia Timu ya Taifa ya Argentina ‘La Albiceleste’ Lionel Andrés Messi amekubali kusaini Mkataba Mpya wa kuendelea kuwatumikia Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain.

Messi mefikia makubaliano na Uongozi wa juu wa Klabu hiyo, kufuatia mkataba wake wa sasa kutarajiwa kufikia kikomo Juni 2023, lakini kulikuwa na kipengele cha kusaini mkataba mpya.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35, tayari alikua anahusishwa na taarifa za kuachana na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu ujao, na kutimkia nchini Marekani kucheza Ligi Kuu ya nchi hiyo MLS.

Taarifa kutoka mjini Paris-Ufaransa zinaeleza kuwa, Messi amekubali kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja, ambao utaendelea kumuweka jijini humo hadi Juni 2024.

Rais wa Paris Saint-Germain Nasser Al-Khelaifi alithibitisha kuwa katika hatua za mwisho za mazungumzo na Lionel Messi, saa chache baada ya Timu ya Taifa ya Argentina Kutwaa Ubingwa wa Dunia Jumapili (Desemba 18) nchini Qatar.

Picha: Rais Mstaafu Alhaji Ally Mwinyi katika Bwawa la Nyerere
Mtoto wa miaka 5 ameza vyuma 52