Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba  ametangaza kujiuzulu uenyekiti ndani ya chama hicho.

Akizungumzia mapema hii leo jijini Dar es salaam, Lipumba amesema amekerwa na hatua ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.

Amesema Ukawa ulianzishwa kulinda maslahi ya wananchi yaliyoainishwa kwenye Katiba iliyowasilishwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba, na kwamba nafsi yake inamsuta hivi sasa kuendelea na uongozi huku waliokuwa wanaipinga Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wa nchi kupitia umoja huo.

Prof. Lipumba amesema baada ya kujiuzulu atajikita kufanya shughuli za kitaaluma kwa kujihusisha zaidi na ushauri wa masuala ya uchumi na maendeleo.

Siri Ya De Gea Kuihama Man Utd Yafichuka
29 Waitwa Kuunda Stars Itakayocheza Dhidi Ya Nigeria