Mwenyekiti wa Chama cha (CUF), anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama ya Siasa Nchini, Profesa Ibrahim Lipumba amesema kuwa CCM na Chadema haviwezi kupambana na ufisadi kwasababu bado vina baadhi ya viongozi ambao tayari walishawahi kutuhumiwa kuhusika na ubadhilifu.
Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa udiwani kata ya kata ya kiwanja cha ndege mkoani morogoro, amesema kuwa CUF ndiyo chama cha kisiasa kinachoweza kupambana na mafisadi, dhuluma na uonevu.
Profesa Lipumba amewataka wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani kupitia chama hicho, Abeid Mlapakolo ili alete mabadiliko katika kata hiyo.amesema kuwa mkoa wa morogoro umejaaliwa kuwa na rasilimali nyingi ikiwamo ardhi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo, lakini wananachi wengi hawanufaiki nazo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari, Sera na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya amesema kuwa kiongozi anatakiwa awe na sifa tatu ambazo ni uadililfu, sera na ufahamu na uwezo na wa kujenga hoja hasa zenye kuleta maendeleo.