Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba ameahidi kuimarisha biashara, kufufua viwanda vilivyokufa na kutoza kodi rafiki kwa wafanyabiashara ili kuinua uchumi wa nchi.

Akiwa mkoani Tanga katika mkutano wa kampeni za Uchaguzi mkuu, Profesa Lipumba amesema “huwezi kuwa na uchumi mzuri bila ya kuwa na mfumo mzuri wa fedha pamoja na ongezeko la ujazo wa fedha ndani ya nchi”.

“Hali ya upatikanaji wa fedha kwa sasa ni ngumu wananchi wanahali ngumu na baadhi ya biashara zinafungwa, CUF mkitupatia rufaa tutafufua viwanda tutaweka mfumo mzuri wa fedha na kuongeza ujazo wa fedha,” amesema Profesa Lipumba.

Aidha CUF inataka kuwepo kwa siasa za amani na kuepuka siasa za vitisho kwa kuwa chama hicho kinaamini katika haki na usawa.

Ukata wakwamisha kampeni za UDP
Kocha Mwadui FC awaita Azam FC