Kocha Mkuu wa Man Utd Erik ten Hag, amebainisha kwamba, beki wake, Lisandro Martínez alikuwa akicheza ingawa hakuwa amepona kwa asilimia 100, kabla ya hivi karibuni kutonesha jeraha lake la msimu uliopita ambapo sasa atakuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili.
Msimu uliopita, Martinez alikosa mechi za mwisho za msimu kutokana na kuumia April 2023.
Akarejea msimu huu ambapo katika mchezo dhidi ya Arsenal wakati Manchester United ikipoteza kwa mabao 3-1, alifanyiwa mabadiliko baada ya kuumia.
Majeraha hayo yamemfanya beki huyo kutoka nchini Argentina kuripotiwa kukaa nje kwa takribani miezi miwili.
“Si habari njema kwa sababu alikuwa anacheza bila ya kuwa amepona kwa asilimia 100,” alisema Ten Hag.
Martinez alikuwa kwenye kikosi wakati timu hiyo ikiruhusu mabao 14 dhidi ya Tottenham, Nottingham Forest, Arsenal, Brighton na Bayern.