Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amesimama kwa mara ya kwanza siku moja baada ya sikukuu ya Krismas.

Lissu alipelekwa jijini Nairobi nchini Kenya kwa matibabu zaidi mara baada ya kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la zaidi ya risasi 20 lililofanywa na watu wasiojulikana.

Aidha, tukio hilo lilijiri mchana wa septemba 7 mwaka huu wakati mbunge huyo wa Singida Mashariki, akitokea Bungeni na kuelekea nyumbani kwake, Area D Mjini Dodoma.

“Leo nimesimama kwa mara ya kwanza, kwa mguu mmoja kwa msaada wa ‘mababa cheza’ hatua inayofuata nitawajulisha,”amesema msemaji wa Lissu huku akinukuu maneno ya mbunge huyo.

Hata hivyo, Lissu amewashukuru madaktari, ndugu jamaa na marafiki na wote walisaidia kuweza kurudi katika hali yake, huku ndugu wakifurahishwa na kitendo cha mbunge huyo kusimama.

 

Video: Mtoto aliyefanyiwa operesheni 10 asafirishwa kwenda India kwa ajili matibabu
Chadema yazidi kupukutika, mwingine aibwaga