Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu nchini Kenya kufuatia kujeruhiwa kwa risasi na watu wasiojulikana siku Septemba 9, 2017 mjini Dodoma amezinduka na kutoa neno kwa Mwenyekiti wa Chama hicho.

Aidha, Katika ujumbe amboa umewekwa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema umesema kuwa kiongozi huyo alipopata fahamu aliweza kutoa maneno machache akimtaka Mwenyekiti kuendeleza mapambano.

Hata hivyo, Lissu bado amelazwa katika hospitali iliyopo jijini Nairobi katika chumba cha uangalizi huku ulinzi ukizidi kuimarishwa katika hospitali hiyo ambayo amelazwa mwanasiasa huyo.

Stoke City yaibana mbavu Man United
Video: Lissu atoa neno baada ya kuzinduka, Serikali yataifisha almasi ya mabilioni