Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye juzi aliachiwa kwa dhamana baada ya kukaa rumande mara mbili, mjini Dodoma na jijini Dar es Salaam, amesimulia hali mbaya iliyomkuta alipokuwa rumande,

Lissu ameeleza kuwa alikumbana na maisha magumu katika rumande zote mbili, huku hali ya rumande hizo ikiwa inatishia afya yake.

Alisema kuwa alipokuwa katika rumande za Chamwino mjini Dodoma hakupata usingizi hata kidogo na kwamba alikutana na mbu ambao hajawahi kuwaona katika maisha yake.

“Sikupata usingizi hata kidogo kutokana na chumba nilicholala kuwa na vumbi na mbu ambao sijawahi kuwaona popote zaidi ya pale,” Lissu anakaririwa na Jambo Leo.

Alisema kuwa alipofika Dar, alikuta hali ni kama ile aliyoIkuta rumande ya Chamwino, lakini hukO aliswekwa ndani na watu wengi kwenye chumba kimoja chenye vumbi jingi na hewa kidogo.

Aidha, Lissu alisema aligundua kitu kimoja kisichokuwa cha kawaida, baada ya kuona watu wanaondolewa rumande nyakati fulani na kwamba alipowauliza wenzake aliambiwa walikuwa wanapelekwa Mikocheni kuteswa.

Mbunge huyo alieleza kuwa baada ya kuwauliza Polisi kuhusu hilo, aliondolewa na kuwekwa kwenye chumba chake peke yake.

Jicho la Lissu lilikiona chumba kile kama sehemu hatari ambayo mtu anaweza kupoteza maisha kwa kukaa humo.

“Ukweli ni kwamba kule si pazuri kwa kumweka mtu kwa maana ni sehemu ambayo mtu anaweza kupoteza maisha,” alisema.

Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema, alisema kuwa ana uzoefu wa kukaa kwenye mahabusu za Polisi, kwani alishawekwa ndani ya mahabusu jijini Arusha na Tarime.

Mwanasiasa huyo anayekabiliwa na kesi za uchochezi, aliliomba Jeshi la Polisi kufanya utaratibu wa kuzisafisha mahabusu zake ili zisiwe hatari kwa afya za watuhumiwa.

Oscar Pistorius akimbizwa hospitali baada ya kupata majeraha Jela
Ubingwa Raha Cheki Lecister City Walivyoenda Mazoezini Jana