Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya Chadema, Tundu Lissu amesema kuwa anaendelea vizuri na atarejea nchini akiwa salama.

Lissu ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio, ambapo amesema kuwa madaktari wamemhakikishia kuwa atarudi nyumbani kuendelea na majukumu yake kama kawaida.

“Madaktari wangu wamenihakikishia kuwa nitarejea nchini na nitaendelea na shughuli zangu kama kawaida,”amesema Lissu

Hata hivyo, katika hatua nyingine Lissu amesema kuwa anachokumbuka katika tukio hilo lililomtokea, wakati wanaingia getini nyumbani kwake mjini Dodoma kulikuwa na gari moja nyeupe ilikuwa imesimama huku kulikuwa na watu wawili.

Ukawa watishia kususia uchaguzi
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 12, 2017