Aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa amesogeza mbele tarehe ya kurudi Tanzania, kutokana na daktari wake kumtaka kuonana naye tena mwanzoni mwa mwezi Oktoba, kwa ajili ya matibabu ya mwisho.

Tundu Lissu ametoa kauli hiyo akiwa nchini Ubelgiji, wakati akizungumzia juu ya mpango wake wa kurejea Tanzania, kama ambavyo alitangaza awali kuwa angerudi Septemba 7.

“Nilisema mwanzoni nitarudi tarehe 7 Septemba, 2019 lakini daktari wangu ameniambia ataniona tarehe 1 Oktoba, 2019 na mara ya mwisho ataniona tarehe 8 Oktoba, 2019, kwa hiyo ile ratiba ya mwanzo haitawezekana, kwa sababu daktari wangu anataka kuniona, Suala la kugombea mwakani halina uhusiano wowote na hii kesi, kwa uchaguzi wa mwaka ujao hakuna chochote cha kunizuia kugombea Ubunge au Urais, kama chama changu na vyama rafiki vitanipa nafasi kukiwakilisha kwenye nafasi hiyo,” amesema Tundu Lissu.

Jana kwenye muendelezo wa vikao vya Bunge jijini Dodoma, Spika wa Bunge Job Ndugai, alimuapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, akichukua nafasi ya Tundu Lissu.

Mahakama ya Afrika Kusini yaamuru kuachiwa kwa ndege ya Tanzania
Mrithi wa Tundu Lissu ala kiapo Bungeni, Janga la vipodozi bandia