Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu  ambaye yuko Nairobi nchini Kenya kwa matibabu, amesema kuwa Bunge la Tanzania halijatoa pesa yoyote kugharamia matibabu yake.

Ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano na moja ya television za hapa nchini, ambapo amesema kuwa hakuna pesa yoyote iliyotolewa na Bunge wala serikali, kwa ajili ya matibabu yake huko nchini Kenya.

“Bunge halijatoa hata senti moja ya matibabu yangu, serikali haijatoa hata senti moja, familia yangu na ndugu zangu inasema mbunge amelazwa tangu Septemba 7, Spika wa Bunge hajaenda, Naibu Spika wa Bunge hajaenda, Katibu wa Bunge hajaenda, Tume ya huduma za Bunge haijaja, haijatoa hata senti 10 kugharamia matibabu yangu”, amesema Tundu Lissu

Hata hivyo, Mnamo Septemba 7, 2017, Mbunge Tundu Lisu alipigwa risasi na watu wasiojulikana, tukio ambalo limemfanya alazwe hospitali kwa zaidi ya miezi mitatu mpaka sasa akipatiwa matibabu, na Bunge lilitoa taarifa kuwa limetuma pesa za matibabu, ambazo hospitali ambayo mbunge huyo akitibiwa ilikiri kuzipokea kwenye acount yake.

Vijana watakiwa kuchangamkia fursa
Polepole: Lema 2020 utalisikia hewani tu jimbo la Arusha Mjini